Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yazindua mkakati zao la mianzi

Kairuki Azindua Kamati Ya Kitaifa Ya Kuongoa Shoroba Serikali yazindua mkakati zao la mianzi

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imezindua mkakati wa kitaifa wa mianzi na mpango kazi wake ikiwa ni hatua ya kulinda viwanda vinavyotumia mianzi kama malighafi na pia kulinda uhifadhi wa maliasili nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki amezindua mkakati huo na utelekezaji wake huku akisema mkakati huo utasaidia upatikanaji wa malighafi kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa zitokanazo na miti ya mianzi.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abassi amezungumzia umuhimu wa kutunza misitu na kuwataka wananchi kuendelea kupanda miti kibiashara ili kujiongezea kipato na kulinda uhifadhi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mianzi Duniani (INBAR) Balozi Ali Mchumo amesem zao la mianzi linaweza kuleta tija kwa Taifa kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya mazao yatokanayo na miti hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live