Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yazindua malipo ya tiketi kwa mtandao

Tiketiiii Onlinee Serikali yazindua malipo ya tiketi kwa mtandao

Fri, 1 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imezindua mpango wa malipo ya tiketi kwa mtandao utakoanza kwa majaribio leo April 1, 2022 nchi nzima kwa lengo la kuboresha huduma za usafirishaji.

Hayo yamesemwa jana Machi 31 jijini hapa na Mkurugenzi wa huduma za uchukuzi wizara ya ujenzi na uchukuzi, Aron Kisaka wakati akiongea na wadau wa usafirishaji katika mikoa ya Manyara na Arusha.

Amesema kuwa, lengo la mkutano huo ni kutoa elimu kuhusiana na elimu ya tiketi mtandao ili wamiliki wote wa mabasi waweze kujua maana ya tiketi mtandao na hatua wanazoweza kuzichukua kuhakikisha wanajiunga na mfumo huo.

Ameongeza kuwa, wataendelea na majaribio hadi June 30 na katika kipindi hicho angalia changamoto na kuzitafutia ufumbuzi ili zikianza kutumika rasmi julai 1 rasmi wamiliki na wadau wote wanaotarajiwa kukata tiketi wawe na elimu hiyo.

"Baada ya kipindi hiki cha majaribio hakuna mtu yoyote anatakayetozwa faini ili hakikisha wote kuwa katika ukurasa mmoja, baada ya kipindi cha majaribio watakuwa Sasa mtu anayefanya makosa anatozwa faini," amesema.

Ameongeza kuwa, wasafiri wengi wanakutana na changamoto wakati wa kusafiri kutana na wapiga debe na kuwauzia tiketi kwa bei ya juu na wakati mwingine wanawauzia gari ambalo haliendi Safari hiyo, ila uwepo wa mfumo huo utawawezesha kulipia kupitia simu za mkononi bila kulazimika kwenda stendi.

Naye Mkurugenzi udhibiti usafiri kutoka mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (Latra), Johansen Kahatano amesema kuwa, hapo awali walikutana na wadau mbalimbali wakiwemo Chama cha wamiliki wa mabasi (Taboa) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa.

Kahatano amesema kuwa, wataendelea kutoa elimu hiyo mkoa wa Dodoma, Mwanza kazi kubwa ikiwa ni kutoa elimu katika kwenda kwenye utaratibu huo mpya huku lengo likiwa ni kuwa na mfumo unaofanana.

Kwa upande wake, Meneja wa Latra Mkoa wa Arusha, Amani Mwakalebela amesema kuwa, Latra mkoa wa Arusha inatarajia kutoa elimu kwa wadau wa usafirishaji na wasafiri ili waelewe mfumo mpya wa ulipaji tiketi kwa njia ya mtandao na njia ya mabenki pindi wanapotaka kusafiri.

Naye Katibu mtendaji kutoka Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro (AKIBOA), Saidi Sharifu amesema kuwa hawakubaliani na mfumo huo kwani wanaona wanataka kutozwa kodi mara mbili katika biashara moja, akisema wanahitaji majadiliano zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live