Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawekeza sekta ya usafiri majini

Meli Nyingine Yashambuliwa Na Wahouthi Wa Yemen Serikali yawekeza sekta ya usafiri majini

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya shilingi Trilioni Moja zimewekezwa na serikali katika kuimarisha sekta ya usafiri majini kwa kununua meli na kukarabati zilizopo.

Mbali na uwekezaji huo, serikali imewataka wadau wa Bahari na Maziwa kuzingatia usalama kwa kuhakikisha vyombo vya usafiri majini vinaendeshwa na watu makini kwa kuzingatia sheria na utaratibu uliowekwa kwa sheria za kitaifa na kimataifa.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema hayo jijini Dar es salam wakati akifunga mkutano wa usalama wa vyombo vya usafirishaji majini chini ya uratibu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania-TASAC.

Chini ya uwekezaji huo, serikali inajenga kiwanda cha meli Kigoma na kujenga meli ya mizigo Ziwa Tanganyika, Mv Mwanza hapa kazi na kukarabati meli katika Ziwa Tanganyika na Victoria na Nyasa.

Pamoja na mambo mengine, Naibu Waziri Kihenzile ameitaka TASAC kusimamia na kuimarisha ulinzi, huku serikali ikiendelea kujenga miundombinu ya kufuatilia kwa karibu usalama katika maji.

Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar, Dokta Khalid Salum Mohammed, huku akitaka juhudi za pamoja katika Bara la Afrika zichukuliwe kwa kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na hali ya usalama katika vyombo vya usafiri Majini.

Lengo la mkutano huo ulikuwa ni kujadili mbinu za kuboresha usalama wa vyombo vya usafiri Baharini, Ziwani na kwenye Mito katika Barani Afrika.

Mkutano huo ulihudhuriwa nchi kutoka Jamhuri ya kidemockrasia ya Congo, Ghana, Madagascar, Afrika Kusini, Cameroon, Nigeria, Kenya, Uganda, Gabon, Uingereza, China, Sweeden na Canada.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live