Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawekeza Bili.500 Bandari ya DSM

Unnamed 1 2 Bandari Bandari ya Dar es Salaam inaendelea na maboresho

Tue, 17 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetoa sh.Bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kuhudumia mizigo ili kuongeza ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) Erick Hamisi wakati wa mkutano wa wadau wa bandari unaofanyika Jijini Tanga ambapo alisema uwekezaji huo unaokwenda kufanyika katika bandari hiyo ni mkubwa

ambao utafungua fursa kwa nchi na maziwa makuu kwa matumizi ya bandari

hiyo.

Alisema kuwa kuna mradi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwara ambapo watapeleka mizigo ya nje katika nchi za Maziwa makuu (Transit) baada ya serikali kuwekeza fedha hizo ambapo pia zitatumika kununulia vifaa ili kuwezesha ufanisi huo.

“Tutakuwa na ujenzi wa bandari ya nchi kavu ya kwara, isitoshe serikali ya awamu ya sita imewekeza kiasi cha shilingi Bilioni 500 kwa mara moja uwekezaji ambao hauajwahi kufanyika kwa mara moja hii inaonesha mhe Rais amedhamiria kuifanya

bandari yetu ifanye kazi kwa ufanisi,” alisema Hamissi.

Mkurugenzi huyo alisema uwekezaji unaofanyika kwasasa katika miundombinu ya reli, Bandari na kwenye maziwa inaoensha kwamba nchi zote zinazotuzunguka

hazitakuwa na chaguo lingine bali kutumia bandari ya Dar es salaam

karibu watu milioni 700 za nchi hizo.

Mkurugenzi huyo alisema mkutano unaofanyika mjini Tanga kuwakutanisha wadau wa bandari haujawahi kufanyika hivyo utatoa fursa kwa wadau kujadili vikwazo na fursa zilizopo katika kuongeza ufanisi zaidi ya bandari zilizopo hapa nchini.

Awali akiungumza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa meli nchini (TASAC)

Kaimu Abdi Mkeyenge alisema kwamba wadau wamekutanishwa pamoja ili

kutazama changamoto wanazokutana nazo kasha waweze kuzipatia majawabu ya

mapendekezo ya kuyafanyia kazi kwa pamoja.

Alisema warsha hiyo itatazama changamoto mbalimbali ambazo zinaipata bandari ya Dare es salaam na fursa zilizopo na kutoa mapendekezo ya kuboresha ikiwemo

bandari ya Tanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa, alisema mkutano huo wa wadau utasaidia kuongeza fursa za usafirishaji mizigo utakaofanywa na shirika hilo ambalo limefanya ukarabati wa reli yake ili kuweza kuhudumia nchi za maziwa makuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live