Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaweka nguvu Mpigachapa Mkuu

WhatsApp Image 2023 08 11 At 10.jpeg Serikali yaweka nguvu Mpigachapa Mkuu

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: Habarileo

SERIKALI imetoa kiasi cha Sh bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kipya cha Mpigachapa mkuu wa serikali na kufufua mashine zilizoharibika na ununuzi wa mashine mpya za kisasa.

Lengo la kujenga kiwanda hicho na kuboresha miundombinu iliyopo ni kuhakikisha usalama wa nyaraka za serikali, ikiwemo kujiendesha kwa ubunifu ili kujiingizia kipato pamoja na utunzaji wa taarifa muhimu za serikali.

Akifungua kikao kazi cha mazingatio ya kazi, ubunifu,utendaji wa kasi ya teknolojia ikiwemo upendo kwa watumishi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama kilichowakutanisha viongozi na watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista amesisitiza lazima nidhamu iwepo pamoja na kuelekeza utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za serikali.

Amesema kiwanda hicho cha Mpigachapa Mkuu wa serikali ni lazima sasa kiongeze maduhuli, kwani kina uwezo wa kupata soko katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mshariki(EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

“Ni wakati sasa wa kiwanda hiki cha Mpigachapa Mkuu wa serikali kujikwamua kiuchumi ikiwemo kupata soko katika nchi za EAC na SADC, ” amesema.

Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Jim Yonazi amesema kikao hicho ni muhimu katika kuongeza tija na kuondokana na utendaji wa kimazoea, ikiwemo kutoa huduma bora kwa wananchi na watumishi mbalimbali wa serikali.

Chanzo: Habarileo