Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imeweka mikakati ya kuwezesha uchumi wa kidijitali.
Mikakati hiyo ni pamoja na kukamilisha uandaaji wa Mkakati wa Taifa wa intaneti yenye kasi na kuandaa Mwongozo wa Kitaifa wa Kushughulikia masuala ya uhalifu wa mtandao.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, wakati akiwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya mwaka 2022/2023 ya Wizara yake mjini Dodoma leo.
Ametaja mikakati mingine ni kuingia mkataba wa ushirikiano na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ili kupunguza gharama za ujenzi wa Mkongo.
“Kuratibu utengenezaji wa mfumo wa kutunza na kuchakata taarifa za kesi na matukio ya uhalifu wa usalama mtandao
“Kukamilisha uandaaji wa rasimu ya Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali, kukamilisha uandaaji wa Mwongozo wa Mageuzi ya Kidijitali.
“Kukamilisha uandaaji wa Programu ya Mafunzo ya TEHAMA, ukamilishwaji wa Mkakati wa Taifa wa Elimu kwa Umma wa Usalama Mtandao,” amesema Nape.