Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawataka wadau kutoa mrejesho upatikanaji wa mafuta, gesi

Gesi Urusii.jpeg Serikali yawataka wadau kutoa mrejesho upatikanaji wa mafuta, gesi

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imewataka wadau mbalimbali kushiriki katika kutoa maoni juu ya upatikanaji wa mrejesho CSR kwenye eneo la mafuta na Gesi Asilia nchini

Hayo yamesemwa leo, Februari 29.2024 wakati wa kikao cha wadau kuhusu kupokea maoni juu ya miongozo ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini, kilichofanyika mkoani Mtwara na kukutanisha wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amesema mwanzo utoaji wa CSR ulikuwa ni utashi lakini hauna sheria, hata hivyo Kwa hao waliokuwa wanatoa walitoa kwa matakwa yao na bila kuzingatia mahitaji halisi ya maeneo husika hivyo kupitia kikao hicho na maoni yatakayo kusanywa yanaenda kutatua changamoto zilizopo

"Kwa sisi Mtwara ambako gesi inatoka fumefarijika kwamba kikao hiki sasa kinaenda kutoa suluhisho la namna ya upatikanaji mzuri wa CSR kwa watu wetu, na nimefarijika kikao hiki kufanyika ndani ya mkoa wa mtwara, kwetu sisi ni fursa" -Kanali Abbas

"Naamini baada ya maoni kukusanywa na kufanyiwa kazi sasa tunaenda kupata sheria iliyokuwa mzuri itakayo elekeza namna ya utoaji wa CSR ikiwa ni pamoja na kushirikisha walengwa kwenye maeneo yao" -Kanali Abbas

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti mkondo wa juu wa Petroli (PURA) Charles Nyangi amesema kikao hicho kina lengo la kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali hasa maeneo ambayo uzalishaji wa gesi asilia yanaendelea na yenye miundombinu

Aidha, maeneo hayo watatakiwa kuandaa miongozo ya uwajibikaji wa makampuni kwenye shughuli za kijamii kwa sababu awali kazi hizo zilikuwa zikifanyika bila kuwepo utaratibu maalum

Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mtwara Selemani Nampanye amesema changamoto zilizopo hapo mwanzo ni wananchi kutoshirikishwa katika utekelezaji wa miradi hivyo amesema kupitia kikao hicho uwazi kwa wananchi utapatikana

Chanzo: www.tanzaniaweb.live