Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawakaribisha wawekezaji kutoka Dubai

Mama Samiapic Data Serikali yawakaribisha wawekezaji kutoka Dubai

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini huku akiwahakikishia mchakato mzima umerahisishwa na unatekelezwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumamosi Februari 26, 2022 wakati akihutubia kwenye Siku ya Tanzania katika maonyesho ya kimataifa ya Expo 2020 Dubai yaliyofanyika Falme za Kiarabu (UAE) huku akiwakaribisha kutembelea banda la Tanzania.

“Nichukue nafasi hii kuwakaribisha wafanyabiashara na wageni wote nchini kwetu, niwahakikishie kwamba kuna mazingira mazuri ya uwekezaji na utalii,” amesema Rais Samia wakati wa hotuba yake.

Amesema wawekezaji ambao watataka kuwekeza nchini, usajili wa kampuni, taratibu za uhamiaji, kupata ardhi, leseni za biashara na kodi, yote yanapatikana katika kituo cha pamoja cha huduma kinachoitwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

“Tanzania imefungua milango yake kwa mtu yoyote atakayetaka kutembea, kuwekeza au kufanya biashara. Inatoa hamasa kubwa ya uwekezaji na mtakutana na roho nzuri za Watanzania; na kwa sababu hiyo tunatabasamu wakati wote,” amesema Rais Samia.

Amesisitiza kwamba serikali itaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Falme za Kiarabu (UAE) kuhakikisha ushirikiano wa kihistoria, kiutamaduni, kiuchumi, kisiasa na kijamii unalindwa na kuendelezwa kwa manufaa ya pande zote mbili.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live