Menu ›
Biashara
Wed, 22 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali kupitia halmashauri, jumla ya vikundi 789 vimepatiwa mikopo mkoani humo katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita.
Wanufaika wa mikopo hiyo ambayo ni zaidi ya shilingi Bilioni nne ni vikundi 420 vya Wanawake, 182 vya Vijana na 187 vya watu wenye Ulemavu.
"Wanavikundi wameweza kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kilimo, ufugaji, karakana za uchomeleaji, mashine za kusaga na ujasiriamali ambazo zinawasaidia kuendesha maisha yao." amesema mkuu huyo wa mkoa wa Kilimanjaro
Chanzo: www.tanzaniaweb.live