Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa ufafanuzi bei ya kununua korosho

39939 Pic+korosho Serikali yatoa ufafanuzi bei ya kununua korosho

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu madai ya watu wa kada mbalimbali, akiwemo mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali kuwa korosho inanunuliwa chini ya Sh3,300 kinyume na agizo lililotolewa na Rais John Magufuli.

Leo Jumatatu Februari 4, 2019 naibu waziri wa Kilimo, Omar Mgumba ametoa ufafanuzi kuhusu bei ya korosho akibainisha kuwa korosho inanunuliwa kwa Sh3,300 kwa kilo moja, kwamba maagizo ya Rais hayajakiukwa.

Mgumba amesema kiasi cha Sh3,300 kwa korosho daraja la kwanza, daraja la pili ndio hununuliwa kwa Sh2,640.

Mgumba alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe aliyetaka kujua kwa nini wanunuzi wa korosho wamekiuka agizo la Rais Magufuli na kuanza kulipa chini ya kiwango ambacho hakikuelekezwa.

Awali Bobali alinukuliwa akisema kwamba atakuwa tayari kujiuzulu ubunge wake iwapo itabainika kuwa wakulima wa korosho wanalipwa Sh3,300 kwa kilo na si Sh2,640.



Chanzo: mwananchi.co.tz