Serikali imefanya maboresho 605 ya kisera, kisheria, kikanuni katika kipindi cha miaka mitano iliyopita 2019 hadi 2023 ili kuvutia wawekezaji.
Hayo yamesemwa leo Februari 27, 2024 na Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo jijini Dar es Salaam katika Jukwaa la Kodi na Uwekezaji.
Amesema, maboresho 416 sawa na asimilia 64 yalilenga kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji nchini.
Pia, maboresha 460 kati ya maboresha 665 yamefanyika kati ya mwaka 2022- 2023 sawa na asilimia asilimia70.
Prof Kitila amesema maboresho hayo yamefanyika ili kuvutia wawekezaji ambao wamekuwa wakiangalia utulivu wa kisiasa na amani katika nchi husika, mazingira ya kisheria hususani kwenye ulinzi wa mali mwekezaji atawekeza kwenye nchi husika.