Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa maagizo wazalishaji vyakula vya mifugo

Ulega Pic Data Serikali yatoa maagizo wazalishaji vyakula vya mifugo

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ametoa rai na kuwasisitiza wazalishaji wa vyakula vya mifugo wote nchini kuhakikisha wanapeleka sampuli za vyakula wanavyozalisha kwenye maabara ya Wakala ya Maabara ya Vetenari Tanzania (TVLA) ili kuhakiki ubora na viwango kwa kuzingatia matakwa ya sheria hiyo kabla ya kuanza kuwauzia wafugaji ndani ya nchi au kuvisafirisha nje ya nchi.

Waziri Ulega alitoa rai hiyo wakati akifungua warsha kuhusu uzalishaji wa protini kwa ajili ya vyakula vya mifugo na kupunguza ushindani iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2023.

Aidha, aliitaka TVLA kuhakikisha inatembelea katika maeneo ya wazalishaji wa malighafi za kutengeneza vyakula vya mifugo ili wakakague ubora wa malighafi hizo ili kuongeza tija na ufanisi wa kazi katika kulinda usalama wa chakula cha mifugo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live