Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa kiasi cha Sh bilioni 20.52 ikiwa ni mkakati wa kuboresha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).
Kiasi hicho kimetumika kulipa sehemu ya gharama za ununuzi wa ndege tano ambapo kati ya hizo, ndege moja ni aina ya Boeing 767-300F ya mizigo, ndege mbili aina ya Boeing 737-9, ndege moja aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na ndege moja aina ya De Havilland Dash 8-Q400.
Ndege nne kati ya 13 hizo zinatarajiwa kuwasili nchini kabla ya Novemba, 2023 na ndege moja ya mizigo inatazamiwa kuwasili nchini hivi karibuni.
Majaliwa amesema kuwasili kwa ndege hizo kutasaidia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutanua mtandao wa safari za ndani na nje ya nchi na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za uchumi kama utalii, biashara na kilimo.
Waziri Mkuu alikuuwa akitoa hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha 2023/24 Bungeni jijini Dodoma.