Menu ›
Biashara
Fri, 24 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Serikali mkoani Tanga, imepiga marufuku pikipiki zilizotolewa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kusimama shughuli za kilimo kutumika kama bodaboda, badala ya kwenda kuhamasisha kilimo biashara kwa wakulima.
Hayo yamesemwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa wakati wa ugawaji wa pikipiki 198 kwa ajili ya maofisa ugani wa wilaya tatu zilizopo mkoani humo.
Amesema lengo la vitendea kazi hivyo ni kuimarisha kilimo biashara, kiweze kuleta tija kwa wakulima sambamba na kuimarisha uchumi wa nchi na sio kutumika kwa matumizi mengine.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live