Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa Tsh. Bilioni 260/- za hisa bomba la mafuta

30918 Pic+bomba Serikali yatoa bil 260/- hisa bomba la mafuta

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI ya Tanzania imetoa Sh bil 259.95 zikiwa ni sehemu ya hisa zake katika mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani,Tanga.

Msimamizi wa ujenzi huo upande wa Tanzania kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Asiadi Mrutu alisema hayo jana wakati akitoa mada ya

fursa za kiuchumi kupitia bomba hilo.

Mrutu alisema fedha hizo ni sehemu ya hisa ya asilimia 15% ya ubia katika mradi huo na kwamba serikali ilizitoa kwa TPDC akiwa ni msimamizi wa mradi kwa upande wa Tanzania.

Alisema kampuni ya Total inamiliki asilimia 62%, kampuni ya mafuta ya Uganda asilimia 15%, TPDC ambayo inaiwakilisha serikali ya Tanzania asilimia 15% huku kampuni ya China CNOOC inamiliki asilimia 8%.

Mrutu alisema kwa upande wa fidia tayari wamelipa takribani Sh bil 1.5 kwa wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa kambi.

“Kwa Mkoa wa Tanga pekee tayari wananchi 81 wameweza kulipwa kiasi cha Sh mil 123.4 kwa ajili ya kupisha ujenzi wa kambi nne ambazo zitajengwa katika wilaya za Handeni, Kilindi, Muheza na Tanga Jiji” alisema.

Aidha Mrutu alizungumzia malipo ya maeneo ambayo bomba litapita wananchi zaidi ya 1, 147 walioko katika

vijiji 48, katika kata 25 zilizoko kwenye wilaya nne ambazo zitaweza kupitiwa na mradi mkoani humo.

Alisema Mkoa wa Tanga unatarajiwa kunufaika na fursa za kiuchumi kupitia bomba hilo katika maeneo mbalimbali ukiwemo ujenzi na huduma za kijamii za chakula na malazi.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima aliitaka TPDC ibainishe maeneo ambayo wananchi wataweza kunufaika moja kwa moja katika mradi huo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz