Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatoa Sh66 bilioni kukarabati barabara korofi

Fedha Ed Serikali yatoa Sh66 bilioni kukarabati barabara korofi

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni 66 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa barabara zilizoharibika nchini.

Fedha hizo tayari zimegawanywa kwa mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa mikoa yote iliyoathirika kwa ajili ya kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili kurekebisha miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha ili shughuli za usafiri na usafirishaji zisikwame.

Akizungumza jijini Arusha mara baada ya kukagua Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha bypass) iliyoharibiwa na mvua hizo, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mohamed Besta amesema fedha za ukarabati wa miundiombinu hiyo zimeshapelekwa mikoa yote nchini.

Mhandisi Besta amesema kuwa tayari kazi inaendelea katika maeneo yote ya nchi na fedha hizo zinaratibiwa na vitengo maalumu vya dharura vilivyopo Tanroads pamoja na ofisi za mikoa.

Ameongeza kuwa kutokana na tathmini iliyofanyika, mpaka sasa zaidi ya shilingi Bilioni 250 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara kuu za mikoa yote nchini.

Amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo kama Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini mwa nchi mvua zimeendelea kunyesha tangu mwezi Oktoba mwaka jana, na sasa unaelekea mwezi wa saba na mvua bado zinanyesha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live