Serikali imetoa fedha Sh milioni 540 kwa ajili ya ujenzi wa majosho mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Ufugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani aliyetaka kujua kauli ya Serikali juu ya ujenzi wa majosho katika Kata za Nyakende, Ulewe, Ubagwe.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Mifugo, Naibu Waziri, Abdallah Ulega amesema Sh milioni 100 zitajumuishwa katika fedha hizo kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo kwenye baadhi ya maeneo nchini.
“Wilaya ya Ushetu ni moja ya wanaufaika naomba mara baada ya hatua hii ya bunge nikutane na Mh Mbunge Cherehani tukutane aweze kunipatia orodha ya vile vijiji vyake kwa ajili ya ufuatiliaji.”amesema Ulega.