Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatishia kuufunga mgodi wa Acacia North Mara

44991 ACCAIANPIC Serikali yatishia kuufunga mgodi wa Acacia North Mara

Wed, 6 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tarime. Serikali imetishia kuufunga mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara endapo mgodi huo utashindwa kupata suluhisho la kudumu dhidi ya tatizo la uchafuzi wa mazingira hususan utiririshaji wa maji ya sumu.

Akizungumza baada ya kukagua miundombinu ya maji machafu mgodini hapo leo Jumanne, Machi 5, Waziri wa Madini, Dotto Biteko ameutaka mgodi huo kuhakikisha kuwa tatizo la maji machafu linapatiwa ufumbuzi kabla ya Machi 30 mwaka huu.

"Serikali haitajali uwekezaji, sisi maisha ya Mtanzania hata mmoja ni ya muhimu mno nyie kwa vile mnafanya biashara, mnatakiwa kuzingatia usalama wa watu wa hapa," amesema Biteko.

Amesema endapo mgodi huo utashindwa kutafuta suluhisho la kudumu juu ya maji hayo yanayodaiwa kutiririka kwenye makazi ya watu basi mgodi huo utafungwa mara moja bila kutoa notisi.

Amesema kuwa tayari Serikali ilishatuma timu ya wataalam kukagua mgodi huo na kwamba tayari walikwishapewa maelekezo juu ya nini cha kufanya kulingana na sheria na taratibu.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa Septemba 7 mwaka jana akitaka mamlaka husika kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wanaozunguka mgodi huo likiwepo suala la maji yenye sumu.



Chanzo: mwananchi.co.tz