Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatia neno matumizi ya Gesi majumbani

7767 Pix 4 Mhe Mgalu TZW

Fri, 11 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Serikali Kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza matarayarisho ya kutekeleza mradi wa kuunganisha gesi majumbani ambapo awamu ya kwanza ya mradi huo umepita katika eneo la Mikocheni Jijini Dar es Salaam.



Akijibu swali la Zainab Mndolwa Amiri aliyetaka kujua, Ni lini Serikali itapunguza bei ya gesi kwa matumizi ya nyumbani kuwawezesha wananchi wengi zaidi kutumia gesi kwa matumizi yao ya Nyumbani, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa Serikali imeendelea kuhamasisha wawekezaji katika sekta ya gesi kwa matumizi ya majumbani.

Mradi wa kusambaza gesi hiyo utaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini lengo likiwa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma hiyo ili kuchochea maendeleo.

“Mpaka sasa Makampuni mengi yameanza kujenga miundo mbinu ya gesi katika sehemu mbalimbali za nchi na kuonesha nia ya kushirikiana na Serikali katika kusambaza gesi asilia nchini,” Alisistiza Mgalu.

Mgalu amesema kuwa kwa hivi sasa gesi inayotumiwa na wananchi kupikia majumbani ni liqudified Petroleum gas ( LPG) ambayo huagizwa na wafanyabiashara kutoka kama ilivyo katika mafuta ya petroli, dizeli, mafuta ya taa na ndege. Aidha gesi hii hujazwa katika mitungi kwa ujazo tofauti.

Aliongeza kuwa mradi wa majaribio wa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya nyumbani ulianza kupitia mradi wa mfano (pilot project) ambapo nyumba 70 zilizoko Mikocheni Jijini Dar es Salaam zimeunganishwa na gesi kwa matumizi ya nyumbani.

Gesi iliyogunduliwa hapa nchini ni Gesi Asilia (Natural Gas) ambayo husafirishwa kutoka kwenye visisima vya gesi hadi kwa watumiaji kupitia mabomba mpaka kwa watumiaji wakubwa wa gesi hapa nchini ni viwanda na mitambo ya kufua umeme.

Loading...
Chanzo: bongo5.com