Serikali imeweka wazi dhamira yake ya dhati ya kuinua kampuni ndogo ndogo na za kati (MSMEs) kwa kuwajejngea uwezo ili kukuza ushindani katika masoko ya ndani na ya Kimataifa kwa kuongeza thamani.
Mpango huo umezinduliwa jana na Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Viwanda Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la maendeleo la umoja wa Mataifa (UNDP) na Mtandao wa Mfuko wezeshi (EIF)
Waziri wa Viwanda na Biashara Kitila Mkumbo ambaye alikuwa ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa mradi huo alisema EIF umefadhili Mradi huo kwa Dola milioni 2.1 za kimarekani na Dola 500,000 za kimarekani zimefadhiliwa na UNDP
Alisema Mradi huo unalenga kusaidia kupunguza ukosefu wa ajira dhidi ya wanawake na Vijana, ambapo mradi huo utatengeneza nafasi za ajira katika maeneo matano ya Asali, Dagaa, Mafuta ya mitende, Bidhaa za urenbo za baharini na Kilimo cha maua.
"Mradi huu umekuja wakati sahihi kwani, tumeanza kutekeleza awamu ya tatu ya Mpango wa maendeleo ya miaka mitano (FYDP 111) ambapo itasaidia kukuza na kurasimisha baadhi ya bidhaa. Alisema Mkumbo.
Utekelezaji wa mradi huo utafanyika Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.