Jumla ya Sh80 bilioni zimetengwa na Serikali kwa ajili ya kudhibiti madhara ya sumu kuvu nchini.
Hayo yamesemwa leo Jumatatu Januari 9 na Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumu Kuvu Tanzania (TANIPAC), Clepine Josephat katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dodoma.
Amesema sehemu ya fedha hizo imetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu kama vile maghala ya kisasa, maabara na vihenge.
“Vijana 400 wamefundishwa kutengeneza vihenge 20 kutoka katika kila wilaya zilizomo kwenye mradi.Pia ujenzi wa maghala bora ili wengine hasa sekta binafsi iige," alisema.
Ametaja baadhi ya wilaya zilizonufaika na ujenzi wa maghala hayo kuwa ni Chemba, Kiteto, Kasulu, Buchosa na Bukombe.
Ameongeza kusema kuwa serikali pia imo.mbioni kujenga maabara ya utafiti wa magonjwa ya kibaolojia.