Hatimaye, serikali imesema itachukua hatua madhubuti juu ya mashamba yaliyotelekezwa ya kilimo cha bustani jijini Arusha ili kukuza na kuendeleza kilimo hico chenye mamilioni ya fedha
Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jumla ya dola milioni 289.6 zilipatikana kutoka kwenye mauzo ya kilimo cha bustani mwaka 2022.
Makusanyo hayo yanatajwa kushuka kutoka $378.6 milioni ambayo iliuzwa nje kwa mwaka uliopita (2021).
Serikali ilisema mashamba mawili ya biashara yatachukuliwa na serikali huku mengine matano yakilazimika kusubiri kwa kuwa bado kuna kesi mahakamani.
Imeongeza kusema kuwa inazingatia malipo yanayotakiwa kutolewa kwa wafanyakazi amabao walikuwa wakidai pesa zao kwenye mashamba hayo mawili yaliyotaifishwa hivyo itakamlisha taribu zote za malipo hayo.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alisema serikali imeamua kuingilia kati ili kurudisha mashamba hayo katika uzalishaji.
Bashe aliyasema hayo akiwa kwenye kitongoji cha Usa River, kitovu cha uzalishaji wa mazao ya bustani katika barabara kuu ya Arusha-Moshi, alipokuwa akijibu hoja za mashamba yaliyoharibiwa.
“Nataka kukuhakikishia; serikali haijashindwa kushughulikia sintofahamu kuhusu mashamba yaliyofungwa,” aliwaambia mamia ya wakazi wa Arumeru, baadhi yao wakiwa hawana kazi baada ya mashamba hayo kutelekezwa.