Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatangaza kumalizana na wakulima wa tumbaku

Tumbaku Malizano Wakulima wa tumbaku kulipwa madai yao

Wed, 18 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wa tumbaku nchini wamehakikishiwa kuwa watalipwa madeni yote wanayodai kampuni za ununuzi wa tumbaku.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Mei 18, 2022 na Makamu mwenyekiti wa bodi ya Tumbaku, Hassan Wakasuvi wakati wa uzinduzi wa barabara ya Tabora Koga hadi Mpanda mjini.

Amesema kuwa wapo baadhi ya wakulima wanaodai na kwamba kilio chao kimesikika na malipo yao yanaandaliwa na muda wowote watalipwa.

"Malipo yenu mnayodai mtalipwa na hata tumbaku mtakayouza nayo itanunuliwa" amesema

Wakasuvi ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, amesema kampuni za ununuzi wa tumbaku zimeongeza kilo za kununua za tumbaku kwa kilo 30 milioni kwa msimu na kuwataka wakulima hao kulima tumbaku kadiri ya uwezo wao.

Advertisement Akizungumzia kuhusu warina asali, amesema wao hawataki nyongeza ya mishahara kwani wataipata katika misitu ya Sikonge na Katavi na wanachokitaka ni changamoto za watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti Wanyamapori na TFS kutokuelewana na wafuga nyuki.

Amesema wafuga nyuki hawataki nyongeza ya mishahara kama wafanyakazi bali kupata asali katika misitu ya Sikonge na Katavi kwa kuwekewa mazingira mazuri ya kufanya kazi yao.

"Mheshimiwa Rais jambo la wafanyakazi tayari lakini bado wafuga nyuki na wakulima" amesema

Wilaya ya Sikonge ni wafugaji wakubwa wa nyuki na mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian amekuwa anahamasisha ufugaji wa nyuki kwa wananchi wa mkoa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live