Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatambua mchango wa sekta binafsi

Shirika Pic Serikali Simanjiro yatambua mchango wa sekta binafsi

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali wilayani Simanjiro mkoani Manyara imesema, itaendelea kutambua na kuthamini michango ya mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yanayo hudumia wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Dk Suleiman Serera amesema hayo jana jumatatu Agosti 21, 2023 kuwa suala la maadili katika utendaji kazi kwa mashirika ni jambo la Kitaifa na Serikali imeyapa uhuru wa kutosha kufanya shughuli zao.

"Suala la maadili ni jambo la Kitaifa.. mashirika mengi tumeyasajili na tumeyaachia yawe huru kuhusu shughuli zao, yaendelee kuzingatia malengo ya kuanzishwa kwao ili kwa pamoja tuweze kujenga jamii moja ya Kitanzania" amesema Dk Serera.

Amesema kwa kufanya hayo changamoto zinazo wakabili wananchi zitapungua na Serikali itahakikisha maendeleo hayo yanakuwa endelevu

Aidha Dk Serera amesema kuna kila sababu ya mashirika kuwa na mijadala na midahalo ya pamoja wananchi na Serikali kujadili changamoto zinazo wakabili wananchi.

"Sasa nitoe rai kwa mashirika na taasisi mbalimbali hapa Simanjiro ambayo yamesajiliwa kwa ajili ya kushirikiana na Serikali kufanya shughuli za kijamii waige mfano wa shirika la CSP Civic Social Protection Foundation la Manyara ambao wameonyesha jitihada za kusaidia wananchi Simanjiro,"amesema

Shirika hilo limetajwa kuisaidia wananchi wa mji mdogo wa Mirerani kuanzisha kituo cha msaada wa kisheria ambacho kinatoa hudumaza kisheria na kuwajengea uwezo wa kibiashara vikundi vya wanawake wajasiria mali wadogo.

Kwa upande wake Obedi Sarakikya ambaye ni msaidizi wa kisheria katika taasisi hiyo amesema kabla ya jamii kuanza kupata elimu ya msaada wa kisheria kulikuwa na ukatili wa haki ya juu wanawake wajasiriamali walivuliwa nguo wakati wa kusachiwa, ukatili wa maneno pamoja na vipigo.

"Hapo awali kulikuwa na ukiukwaji mkubwa sana wa sheria kama vile ukaguzi usiokuwa na staha, ukatili wa maneno hali iliyokuwa inadhalilisha utu wa mtu"amesema Obedi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live