Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatakiwa kuwa makini ushuru ngano, mafuta

Ngano Ngano Serikali yatakiwa kuwa makini ushuru ngano, mafuta

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Maswa Mashariki (CCM) Stanslaus Nyongo ametaka Serikali kuwa makini katika suala la ushuru kwenye mafuta ya kupikia na ngano kwasababu wakicheza vibaya watakwenda kuwaumiza wananchi. Nyongo ameyasema hayo leo Jumatano Juni 21, 2023 wakati akichangia hali ya uchumi, Mpango wa Maendeleo wa Taifa na bajeti ya mwaka 2023/24. Amesema wabunge wengi wamepiga kelele baada ya kusikia kuwa Serikali inakwenda kupunguza bei ya mafuta ghafi yanayoingizwa kutoka nje ya nchi na kwamba mafuta ya chikichi siku zote ni gharama rahisi.

Mbunge wa Maswa Mashariki (CCM) Stanslaus Nyongo ametaka Serikali kuwa makini katika suala la ushuru kwenye mafuta ya kupikia na ngano kwasababu wakicheza vibaya watakwenda kuwaumiza wananchi. Nyongo ameyasema hayo leo Jumatano Juni 21, 2023 wakati akichangia hali ya uchumi, Mpango wa Maendeleo wa Taifa na bajeti ya mwaka 2023/24. Amesema wabunge wengi wamepiga kelele baada ya kusikia kuwa Serikali inakwenda kupunguza bei ya mafuta ghafi yanayoingizwa kutoka nje ya nchi na kwamba mafuta ya chikichi siku zote ni gharama rahisi. “Ukileta kwa bei ambayo umempunguzia kodi huyu mwagizaji mafuta ghafi ya chikichi, muuzaji wa mafuta ya chikichi, pamba, alizeti hawezi kuingia katika ushindani kwasababu mafuta yake yatauzwa kwa bei ya juu,” amesema. Amesema ukiweka kodi ya asilimia 35 kwa muagizaji wa mafuta ghafi ya chikichi yanayoagizwa kutoka nje, atasafisha mafuta na mabaki yake yatatengeneza sabuni. Amesema muagizaji huyo atapata faida kwenye mafuta na sabuni lakini kwa mtengeneza mafuta ya alizeti na pamba anachopata ni mashudu ambayo ni chakula cha wanyama. “Tujaribu kukaa na kufikiria kuona ni namna gani ya kufanya ili kusudi Mtanzania asije akanunua mafuta kwa bei ya juu. Kwasababu mgogoro wa mafuta unakwenda hadi kwa muuza chips. Unakwenda kwa Watanzania moja kwa moja,”amesema. “Tuangalie namna ya kufanya, vile vile kwenye ngano kuna mbunge mmoja amepiga kelele sana. Mahitaji ya ngano kwa mwaka ni metriki tani milioni moja na uzalishaji wetu ni asilimia 20 tu. Hatuwezi kuishi bila kuagiza ngano,”amesema. Amesema Wizara ya Kilimo iweke sharti kwa waagiza ngano kuwa asilimia 20 hadi 30 ya ngano anayonunua anunue ndani ya nchi. “Lakini mkipandisha sana kodi madhara yanakwenda moja kwa moja kwa mama ntilie anapika chapati, ikibaki inaliwa mchana na ikibaki anakwenda kuwapa wanane wale mchana,” amesema. Nyongo amesema ngano imekuwa chakula kikubwa na pia chips zinazokaangwa na mafuta imekuwa ni chakula kinachoshindana na wali. “Ni lazima tuwe makini tukicheza vibaya tukakuta kodi imepanda athari inakwenda kwa Mtanzania moja kwa moja kwa hili lazima tuwe makini na kuweza kuishauri vizuri Serikali,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live