Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataka ukaguzi wa mbegu zinazosambazwa

Mbeguuu Mbeguuu.png Serikali yataka ukaguzi wa mbegu zinazosambazwa

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde ameitaka Taasisi ya Uthibiti na Udhibiti wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kuhakikisha inaweka mkazo mkubwa kwenye ukaguzi wa mashamba ya mbegu ili kuhakikisha mbegu zinazosambazwa kwa wakulima kuwa ni mbegu bora zitakazoleta leta tija katika uzalishaji.

Mavunde ameyasema hayo leo Machi 15,2023 alipotembelea na kukagua utekelezaji wa majukumu wa TOSCI.

Amesema tasnia muhimu haitaweza kujitosheleza kwa chakula au kufikia malengo yaliyowekwa katika uzalishaji wa mazao pasipo kuwa na uhakika wa mbegu bora.

"Serikali yenu inayoongozwa na mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuongeza uwekezaji kwenye utafiti na uzalishaji wa mbegu bora nchini ili tuweze kufikia malengo makuu ya kukuza kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.'Amesema Mavunde

Amesema ni lazima TOSCI itimize jukumu la kubwa la kuhakisha mashamba ya uzalishaji ya mbegu yanakaguliwa,kwasababu wao ndio wenye dhamana ya uthibiti na udhibiti wa mbegu hapa nchini.

"Rai yangu kwenu ni kuimarisha ukaguzi ili mkulima anufaike na mbegu bora."

Amesema serikali itahakikisha inaendelea kuwekeza katika vifaa na miundombinu bora ili kurahisisha jukumu hilo sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa TOSCI ili waweze kutekeleza majukumu yao kiufanisi kwa kufuata misingi ya utaalamu wa kazi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live