Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataka BoT kuuziwa dhahabu

Wezi Waiba Dhahabu Ya Sh Bil. 3.8 Serikali yataka BoT kuuziwa dhahabu

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NAIBU Waziri wa Madini, Dk Stephen Kiruswa ameitaka kampuni ya mgodi wa Bucreef Gold Company (BGC) kuangalia uwezekano wa kuanza kuiuzia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) dhahabu yote wanayoizalisha.

Dk Kiruswa ametoa maelekezo hayo alipotembelea mgodi huo uliopo Kata ya Lwamugasa wilayani Geita, ambapo serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) inamiliki hisa kwa asilimia 45.

Amesema biashara hiyo inawezekana kwani mwezi Septemba mwaka huu, BoT ilitangaza kuanza kununua dhahabu kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa ndani kama sehemu ya kuhifadhi fedha za kigeni.

Kiruswa ameelekeza Bucreef kufanya mapitio ya mikataba waliyoingia na wanunuzi wa nje na kuangalia kama haiwafungi basi waunge mkono hatua hiyo ya serikali ,ili kuiwezesha BoT kufikia malengo yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live