Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataja hatua tisa kuongeza Dola sokoni

Dola Dola Juu Juu Serikali yataja hatua tisa kuongeza Dola sokoni

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetaja hatua tisa zenye matumaini ya kuimarisha huduma ya Dola ya Marekani katika mzunguko wa soko baada ya kusababisha mshtuko kwa zaidi ya miezi kadhaa nchini. Hatua hizo ni pamoja na kuanza kuweka akiba ya dhahabu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuongeza utafutaji wa mikopo, kuweka dhamana katika bidhaa zinazouzwa nje, BoT kufanya biashara ya kuuza dola, utoaji wa leseni za maduka ya kubadilishia fedha na kuongeza hamasa ya mauzo ya bidhaa nje. Hatua zingine ni kila mtanzania kutumia shilingi ya Tanzania kwenye Manunuzi ya huduma na bidhaa nchini, utoaji wa taarifa za masoko yasiyokuwa rasmi ya dola na kuwezesha wafanyabiashara kwa kuwapatia shilingi ili kuleta dola nchini kama mbinu ya kuongeza dola kwenye mzunguko nchini.

Serikali imetaja hatua tisa zenye matumaini ya kuimarisha huduma ya Dola ya Marekani katika mzunguko wa soko baada ya kusababisha mshtuko kwa zaidi ya miezi kadhaa nchini. Hatua hizo ni pamoja na kuanza kuweka akiba ya dhahabu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuongeza utafutaji wa mikopo, kuweka dhamana katika bidhaa zinazouzwa nje, BoT kufanya biashara ya kuuza dola, utoaji wa leseni za maduka ya kubadilishia fedha na kuongeza hamasa ya mauzo ya bidhaa nje. Hatua zingine ni kila mtanzania kutumia shilingi ya Tanzania kwenye Manunuzi ya huduma na bidhaa nchini, utoaji wa taarifa za masoko yasiyokuwa rasmi ya dola na kuwezesha wafanyabiashara kwa kuwapatia shilingi ili kuleta dola nchini kama mbinu ya kuongeza dola kwenye mzunguko nchini. Serikali inataja hatua hizo ikiwa ni miezi kadhaa ya mshtuko wa sarafu hiyo katika mataifa mengi, hususan ya Afrika ambayo yana utegemezi mkubwa wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kuwa sarafu hiyo ya Marekani inahusika kwa asilimia 85 katika miamala yote ya kimataifa. Akizungumza na wanahabari leo Agosti 26, 2023, Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema sababu iliyoathiri ni mabadiliko ya sera za Marekani yaliyohusisha kiwango kikubwa cha sarafu hiyo kuelekezwa kwenye uwekezaji huku Benki Kuu ya Marekani ikiongeza viwango vya riba kwa asilimia 0.25. Kwa mujibu wa BoT, hadi Agosti 23, mwaka huu akiba ya fedha za kigeni ilikuwa Dola za Marekani 5.41 bilioni ambayo inatosha kuagiza bidhaa za nje kwa miezi minne na siku 27. Asilimia 77 ni Dola za Marekani, asilimia 16 Yuani ya China, asilimia 4.78 Pauni ya Uingereza na asilimia 1.72 Dola ya Australia. Akifafanua kuhusu hatua hizo, Msigwa amesema tayari Serikali imeanza kutekeleza sera yake ya fedha ununuzi ya dhahabu kama akiba ya fedha kupitia BoT. “Ukinunua dhahabu baadaye ukiuza unapata dola, sasa tumeshaanza, kati ya Mei hadi Julai tumenunua kilo zaidi ya 400 zilizohifadhiwa BoT.” Pili, amesema Serikali imeongeza utafutaji wa mikopo itakayokuwa kwenye thamani ya dola kisha kuipeleka katika mzunguko wa soko nchini ili kupunguza presha ya uhaba huo. Tatu, ni kutoa dhamana kwa bidhaa zinazouzwa nje ili kuongeza kiwango cha dola nchini pamoja na kuwawezesha wazalishaji wa ndani ili kuongeza mauzo ya nje. “Tunahitaji kuongeza mauzo ya nje ili kuongeza dola nchini, Serikali inaendelea kusaidia waalishaji wa ndani.” Tano, Msigwa amesema BoT imeanza kuuza dola kwa taasisi za kifedha nchini, akisema tayari dola milioni 20 zimeuzwa jana kwa benki nchini kwa ajili ya kuingiza kwenye mzunguko wa soko. Sita ni kuongeza idadi ya maduka ya kubadilishia fedha, akisema tayari Serikali imeshatoa leseni 80 za maduka huku akitoa hamasa ya kujitokeza wafanyabiashara wenye mpango wa kufanya biashara hiyo. “Hata yale tuliyokuwa tumeyafungia awali, baada ya kukidhi vigezo sasa tumerejeshea leseni zao. Wale ambao hawakutimiza wameelekezwa watimize masharti, wako pia fedha zao zilichukuliwa sasa Serikali imeshafanya tathmini na baadhi yao wamerejeshewa fedha zao karibu Sh9bilioni,”amesema Msigwa. Msigwa amesema jambo la msingi ni kuendelea kuhamasisha uzalishaji wa ndani hususani bidhaa za kilimo kwa ajili ya kukuza mauzo ya nje, ambazo kwa sasa zinachangia asilimia 25 ya fedha za kigeni. “Serikali imetoa maelekezo kwa wizara zote kuhakikisha Jambo la nane ni kuhakikisha kila mtanzania anatumia shilingi ya Tanzania katika miamala yote huduma na bidhaa nchini badala ya dola ikiwa ni utekelezaji wa waraka wa BoT. “Vyombo vyetu vinafuatilia watakaobainika watachukuliwa hatua,”amesema. Tisa ni kushirikiana na Serikali katika utoaji wa taarifa za masoko yasyokuwa rasmi ya dola inayoingiza fedha kwa njia zisizokuwa halali pamoja na kuondoa fedha nchini kwa njia zisizokuwa halali. “Lakini hali inaimarika, mfumuko wa bei Marekani umeshaanza kupungua kutoka asilimia nane iliyokuwa imefikiwa hadi sasa asilimia tatu, matarajio hadi mwisho wa Desemba utakuwa umeshuka hadi asilimia mbili hivyo kulegeza mkakati wa kukusanya dola zake kuingia Marekani,”amesema Msigwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live