Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataifisha Tanzanite, yafunga mgodi

Tanzanite Mnkl.jpeg Serikali yataifisha Tanzanite, yafunga mgodi

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Madini imetaifisha madini ya tanzanite yenye uzito wa kilo nne yenye thamani ya mamilioni ya fedha ya mgodi wa Kitalu C unaomilikiwa na serikali na mwekezaji mzawa, Onesmo Mbise.

Inadaiwa kuwa madini hayo yametaifishwa kutoka kwa Meneja wa mgodi wa Gem & Rock Venture, Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti.

Hayo yalisemwa na Ofisa Mfawidhi Wizara ya Madini Mkoa wa Manyara, Mernad Msengi na kusema kuwa thamani halisi bado haijajulikana ya madini hayo ya tanzanite yaliyochimbwa kwa njia haramu na Saitoti akiwa na wafanyakazi wake walioingia kitalu C Machi 12, mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live