Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataifisha Ng'ombe 68, ndama watatu

Mifugo Ya Ngombe 620x308 Serikali yataifisha Ng'ombe 68, ndama watatu

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara imeamuru ng'ombe 68 pamoja na ndama watatu kutaifishwa kuwa mali ya Serikali baada ya kukamatwa wakichungwa katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire eneo la Sanjaweda Babati Mkoa wa Manyara.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Victor Kimario baada ya Washtakiwa watano kukutwa na hatia ya makosa mawili ambayo ni kuingiza mifugo ya nyumbani katika Hifadhi ya Taifa pamoja na kufanya uharibifu asilia kwa kuingiza mifugo hiyo kwenye Hifadhi.

January 20, 2023 Washtakiwa hao ambao ni Manakei Hanoti (17) Gwanyangwa Hanoti (21), Paulo Ngeresi (24), Shabani Kamaza(26) na Madei Ngahe(23) walikutwa na Askari wa Uhifadhi wa Tarangire wakilisha mifugo yao katika eneo la Hifadhi ambapo walikuwa ng'ombe 68 huku ndama watatu wakizaliwa baada ya kushikiliwa.

Mahakama kwa kuzingatia pande zote mbili, Hakimu Kimario amewahukumu kifungo baridi(nje) cha miezi minne Kila mmoja kwa kosa la kwanza pamoja na kifungo cha mwezi mmoja kwa kosa la pili ambapo hawatatakiwa kufanya kosa lolote la jinai kuanzia sasa katika kipindi hiki cha adhabu huku mifugo hiyo ikitaifishwa kuwa mali ya Serikali na kupigwa mnada, ambapo haki ya kukata rufaa ipo ndani ya siku 30 kuanzia leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live