Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yasitisha uwekaji hereni mifugo

Hereni Ngombe.jpeg Serikali yasitisha uwekaji hereni mifugo

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesitisha kwa miezi mitatu shughuli ya utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kieletroniki ili kutoa muda wa kufanya tathimini ya kazi hiyo.

Hayo yamesemwa leo, Alhamis Novemba 3, 2022 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo bungeni jijini Dodoma.

Majaliwa amesema Serikali imesikia hoja za wafugaji kuhusu mapungufu wa kanuni, usimamizi wake na utekelezaji wake na gharama kubwa ya uwekaji wa hereni za kielektroniki na hivyo kuona kuna haja ya kufanya upya tathmini ya kazi hiyo.

“Serikali imeamua kusitisha utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kielektroniki kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka Januari 31, 2023 wakati ikiendelea na tathmini ambayo itawezesha kutoa mwongozo wa namna bora zaidi ya kutekeleza zoezi hilo kwa mafanikio,”amesema.

Amesema utambuzi kwa hereni ulipaswa kukamilika Oktoba 31,2022 lakini tangu kuanza kwa utekelezaji wa kanuni husika mwaka 2021 hadi kufikia tarehe hiyo idadi ya mifugo iliyowekwa hereni ni milioni tano tu imetambuliwa na kusajiliwa sawa na asilimia 11 tu ya lengo la lengo la kutambua mifugo milioni 45.9.

Majaliwa amesema kufuatia hali hiyo Serikali ilitoa taarifa kwa umma kuongeza muda wa utambuzi kwa hiyari Desemba 31, 2022 na baada ya hapo ingechukua hatua za kisheria kwa wasioweka.

Amesema bei elekezi ni Sh1,750 kwa ng’ombe na punda Sh1,000 kwa mbuzi na kondoo, gharama ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wafugaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live