Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yasitisha ukaguzi wa risiti za EFD

Mwigulu Kitila Dfgb Serikali yasitisha ukaguzi wa risiti za EFD

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.

Hayo yamesemwa kwa niaba ya Serikali, jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara.

Kikao hicho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live