Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yasajili wakulima milioni 1.9

Bashe Serikali yasajili wakulima milioni 1.9

Mon, 5 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Aidha mikoa mitano ya Morogoro,Njombe,Mara,Tabora na Kilimanjaro imeongoza kwa kusajili wakulima wengi kwenye Mfumo wa M-Kilimo ulioanza kufanya kazi ya kuwatambua wakulima wake hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo huo namna unavyofanya kazi katika sekta ya Kilimo.

Naibu Waziri Bashe amesema wakulima wamesajiliwa katika mfumo huo,wameweza kuwasiliana ikiwemo kuuliza maswali na kupata majibu ya changamoto za uzalishaji na masoko ambazo zinawakabili.

Amesema mfumo huo umewezesha kusajili maafisa Kilimo katika ngazi zote kuanzia sekretarieti za Mikoa,Halmashauri za Wilaya,Kata na Vijiji.

“Mfumo huu utasaidia kupima utendaji kazi wa maafisa Ugani Kilimo katika maeneo mbalimbali," amesema.

Chanzo: ippmedia.com