Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapunguza tozo bandari ya Tanga, Mtwara

Bandari Bagamoyo Serikali yapunguza tozo bandari ya Tanga, Mtwara

Thu, 19 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ili kuvutia na kuendeleza bandari za Tanga na Mtwara Serikali imepunguza tozo kwa kiwango cha asilimia 30, ili bandari hizo ziweze kupata meli zinazoshusha mizigo ili kuzisaidia nchi zilizo karibu na bandari hizo.

Majaliwa ameyasema hayo leo katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma leo Mei 18, 2022, na kusema kuwa lengo la kupunguza tozo hizo ni pamoja na kuvutia nchi jirani kama Uganda, Sudan Kusini na Malawi

"Tumefanya mapitio ya tozo hasa kwa bandari ya Tanga na Mtwara tumetoa fursa ya tozo ili kuwavutia wafanyabiashara na kuipunguzia mzigo bandari ya Dar es Salaam na tuna amini kwa hili tutawavutia wengi" Majaliwa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live