Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapunguza makali ya mafuta

Mafuta Ya Petrol Serikali yapunguza makali ya mafuta

Fri, 8 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura) imetangaza bei mpya za mafuta huku lita moja ya petroli ikiongezeka kwa Sh183.

Bei ya petroli imeongezeka kutoka Sh2, 459 kwa mwezi Machi hadi Sh2, 642 sawa na ongezeko la asilimia 7.44.

Hata hivyo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kupunguza makali ya bei kwa kufidia Sh250 kwa kila lita ya mafuta.

Bei ya dizeli itauzwa kwa Sh2, 644 ikilinganishwa na Sh2500 ya Machi sawa na ongezeko la Sh144.

Akitoa taarifa ya mabadiliko ya bei hizo leo Ijumaa Aprili 8, 2022, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Zura, Mbaraka Hassan Haji amesema mabadiliko hayo yanatokana na mambo mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya bei duniani.

Amesema katika mabadiliko ya bei hizo zinazoanza kutumika kesho Aprili 9, lita moja ya mafuta ya taa imeongezeka kwa Sh362 kutoka Sh1, 811 hadi Sh2, 173 sawa na asilimia 20.

"Mabadiliko haya yanazingatia gharama za usafiri, Kodi za Serikali, gharama za uingizaji wa mafuta katika bandari ya Dar es Salaam na wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei duniani," amesema

Zanzibar inaingiza wastani wa lita za mafuta milioni 18,000,000 kwa mwezi.

Juma Hassan Mkazi wa Mpendae Unguja, amesema ipo haja Serikali kuzidi kuingilia zaidi suala hilo maana gharama za maisha zinapanda kwa kasi.

"Ni sawa inachangia kwa kiasi kwenye punguzo lakini bado gharama hizi ni kubwa na wala sio kwamba zinawagusa wenye magari peke yao hata Mwananchi wa kawaida maana mafuta yakipanda kila kitu kinapanda," amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live