Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapunguza gharama daraja la Nyerere Kigamboni

DARAJA Kigamboni.jpeg Serikali yapunguza gharama daraja la Nyerere Kigamboni

Mon, 23 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Serikali imesikia kilio cha wananchi juu ya malipo ya kuvuka daraja la Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar es Saalam na kubadili mfumo wa malipo ambao unaelezwa utakuwa na ahueni.

Watumiaji wa daraja hilo sasa wataweza kufanya malipo ya siku (mara moja) bila kujali watapita mara ngapi wakati malipo ya wiki na mwezi yakisubiri kukamilika kwa marekebisho ya mifumo.

Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile alisema kilio cha wakazi wa Kigamboni ni tozo hizo kuondolewa kabisa.

Amesema kuanzia sasa baadhi ya tozo zitakazokuwa zinatozwa ni ile ya bodaboda bei itakuwa Sh300 kwa safari, Sh500 kwa siku, Sh2, 000 kwa wiki na Sh5, 000 kwa mwezi,” ameeleza Dk Ndugulile.

Awali bodaboda katika eneo hilo zilikuwa zikilipia Sh600 kila zilipopita jambo ambalo lilikuwa likilalamikiwa.

Bajaji sasa zitalipa Sh500 kwa safari, Sh3,000 kwa siku, Sh10,000 kwa wiki na Sh20,000 kwa mwezi hii ni kutoka Sh1,500 iliyokuwa ikilipishwa awali kwa kila safari kwa baiskeli za miguu mitatu yaani guta, mikokoteni na bajaji.

Magari madogo sasa yanalipia Sh1,500 kwa safari, Sh2,500 kwa siku, Sh12,000 kwa wiki na Sh35,000 kwa mwezi ikilinganishwa na Sh1,500 iliyokuwa inatozwa kwa kila safari katika daraja hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live