Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapongezwa kuingia uchumi wa kati

Banc Abc1 Serikali yapongezwa kuingia uchumi wa kati

Tue, 7 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BANCABC imeipongeza serikali kwa kuwezesha nchi kuingia kwenye uchumi wa kati na kuahidi kuendelea kutoa huduma za mikopo zenye riba nafuu kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa ili waweze kukuza biashara zao.

Mkuu wa Kitengo cha Hazina ndani ya benki hiyo, Barton Mwasamengo, aliyasema hayo jana katika maonyesho ya 44 ya biashara yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mwasamengo alisema benki hiyo inaunga mkono juhudi za serikali za kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati kwa kuwawezesha wafanyabiashara wa aina zote kupata fursa ya mikopo ya riba nafuu.

Pia alisema kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona ambayo imekumba nchi mbalimbali duniani, benki yake katika kumjali mteja wanaangalia namna ya kumpa unafuu wa kurejesha mkopo.

"Kwa wateja waliokopa na ambao hawajakopa tumefungua milango hasa kutokana na janga hili la corona tumekuwa tukiwapa unafuu wa riba wa namna ya kurejesha mikopo yao," alisema.

Alisema wanatoa mikopo ya watu binafsi ili kuendeleza shughuli ndogo ndogo kama za mama lishe.

Alisema katika maonyesho hayo wamelenga kuonyesha bidhaa za mikopo wanayoitoa, kufungua akaunti ambayo kila mwezi inapata riba kwa mwenye salio kuanzia Sh. 10,000, haina makato ya kila mwezi na haina kima cha chini cha kuendesha akaunti.

Pia alisema wanafanya huduma za kibenki kidigitali ambazo mtu ahitaji kuwa na akaunti na anaweza kufanya ununuzi kupitia mtandao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live