Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapokea matrekta 500, pewer tiller 900

Trekta Aaaa (600 X 317) Serikali yapokea matrekta 500, pewer tiller 900

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imepokea matrekta 500 na power tiller 900 na vifaa vingine 200 vya kilimo kutoka kampuni ya Kitanzania ya Agricom.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye alishuhudia makabidhiano hayo wakati wa maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika Dodoma jana Alhamisi Agosti 8, 2024.

Makabidhiano haya ni sehemu ya mpango wa Serikali wa agenda 10/30 ya kilimo ni biashara, unaolenga kuboresha kilimo nchini kwa kuwapatia wakulima zana bora zinazoongeza ufanisi na uzalishaji.

Zana hizo zinatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya kilimo, kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa na kuimarisha usalama wa chakula nchini Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live