Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapiga ‘stop’ uingizaji vifaranga

Images (19) Vifaranga.jpeg Serikali yapiga ‘stop’ uingizaji vifaranga

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania imesema, haitaruhusu kuingiza vifaranga vya kuku nchini na haitatoa tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo kuaniza Julai 30, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Jumamosi Julai 23, 2022 imesema Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema baada ya Julai 30, hakuna vifaranga vya kuku vitakavyoingizwa hapa nchini na Serikali haitoi tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo.

Taarifa hiyo imesema, Ulega amebainisha hayo jijini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku, kujadili namna ya kukuza tasnia hiyo,

Lengo la hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria ya mwaka 2006 ambapo Serikali imekuwa ikizuia uingizaji wa vifaranga nchini kutoka nje ya nchi ili kudhibiti ugonjwa wa mafua ya ndege kwa mifugo jamii ya ndege na kulinda wazalishaji wa kuku ndani ya nchi.

Akifungua kikao hicho kilichojadili ajenda mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na bei ya kuku sokoni, Ulega amesema Serikali inategemea haitaona vifaranga vinaingizwa nchini kutoka nje ya nchi.

Ametaka kuwepo kwa mfumo wa taarifa zinazohusu wazalishaji wa vifaranga vya kuku kuanzia wazalishaji wakubwa hadi wadogo ambao wamesajiliwa na kutoa taarifa serikalini ili kuiwezesha kujua kiwango cha uzalishaji na kuwa na takwimu sahihi juu ya mahitaji ya vifaranga nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live