Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapiga marufuku usafirishaji wa nguruwe

Ngureweeeee Serikali yapiga marufuku usafirishaji wa nguruwe

Sat, 5 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Aidha, kata tano kati ya 29 za Manispaa ya Morogoro zimethibitika kuathiriwa na ugonjwa huo.

Ofisa Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Dk. Petro Lema, alithibitisha hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa ugonjwa huo hauna madhara kwa binadamu atakekula nyama ya nguruwe aliyeathiriwa.

Alisema walipata taarifa ya kuibuka kwa ugonjwa huo Juni 2 na kuchukua sampuli kuzipeleka maabara ya chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na kubaini kuwapo kwa vimelea vya ugonjwa huo kwa nguruwe waliokufa katika kata za Kingolwira, Tungi, Kichangani, Boma na Kilakala.

Dk. Lema alisema uchunguzi wa awali wamebaini kuwa ugonjwa huo kutokea mkoani Dodoma na Manispaa ya Morogoro ulianzia kata ya Kingolwira na idara ya mifugo kwa kushirikiana na jeshi la polisi  tayari wameshaweka vizuizi katika mpaka wa barabara ya Iringa, Dodoma na Dar es salaam ili kuzuia wafanyabiashara kuingiza au kutoa wanyama hao.

Alisema wanaokula nyama hiyo kwenye vibanda, mabucha na baa hawaruhusiwi kubeba mabaki kupelekea mifugo nyumbani ili kuepuka ugonjwa huo kusambaa.

“Tumeendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali wakiwamo wauzaji wa kitoweo cha nguruwe, wafugaji na wauzaji chakula cha mifugo, ugonjwa huu unasababishwa na kirusi na hautibiki,” alisema.

Pia, alisema atakayekiuka masharti atachukuliwa hatua ikiwamo kutozwa faini ya Sh. 200,000 na watakaobainika kuwa na nyama hiyo bila mihuri, nyama itateketezwa.

Chanzo: ippmedia.com