"Marufuku mifugo kuingizwa katika maeneo ya misitu au yaliyopandwa miti ili kuepuka uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira"- Waziri wa Maliasili na Utalii Baloz Pind Chana
Waziri Pindi Chana ametoa maelekezo hayo leo Januari 11 jijini Dodoma wakati akishiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Swaswa ikiwa ni njia ya kusheherekea miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar ambapo Wizara ya Muungano na Mazingira imeagiza upandaji miti maeneo mbalimbali kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha, amesema kuna changamoto nyingine ya suala la moto kutokana na shughuli za binadamu kuongezeka kwenye maeneo ya hifadhi kwa kusafisha mashamba kwa kuchoma badala ya kutumia njia mbadala.