Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapiga marufuku manunuzi ya 'Kangomba' kwenye korosho

Korosho 2aaz Serikali yapiga marufuku manunuzi ya 'Kangomba' kwenye korosho

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda ametoa onyo kali kwa wanunuzi wa korosho kwa njia isiyo halali maarufu kama 'kangomba'.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya maafisa ushirika yanayojumuisha mikoa mitano yanayofanyika mkoani mtwara amesema kuwa lazima wakemee mtindo huo ili kumsaidia mkulima.

"Kangomba imerudi na inampiga mkulima kwelikweli, naomba viongozi wote tusaidie kuwalinda wakulima, jamani tusaidianeni kuhimiza wakulima wasikubali kangomba, na wale mnaonunua kwa mtindo huu mjue mnawadidimiza wakulima" Waziri Mkenda.

Waziri huyo amewasisistiza wakulima kuhakikisha wanakwepa mfumo huo kwa hauna manufaakwa taifa na unawarudisha nyuma wakulima kwa kiasi kikubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live