Wilaya ya Same ni moja ya wilaya nchini inayolima zao la tangawizi kwa wingi pamoja na kilimo cha mpunga,licha ya kuwa wakuliwa wengi wanakabiliwa nanchangamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa mbolea.
Serikali kupitia wizara ya kilimo baada ya kupokea ukubwa wa kero hiyo kutoka kwa mbunge wa Same mashariki Anna kilango Malecela imepeleka Tani 148 katika jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya kuwanusuru wakulima wa zao la tangawizi na mpunga katika eneo hilo.
Mbolea hii ya ruzuku imeanza kutolewa kwa wananchi wa tarafa tatu, kata 14 yenye vijiji 49 na ambayo utakwenda kuongeza uzalishaji katika eneo la kilimo ambacho wananchi wamekua wakiteseka kutokana na ukosefu wa mbolea.
Mbolea hii inatolewa kulingana na bei elekezi ya serikali na wananchi wanaelezea furaha yao juu ya ujio wake.