Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapanga kuboresha sekta ya Mifugo

Picha 1 1 1140x640.jpeg Serikali yapanga kuboresha sekta ya Mifugo

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini, imeahidi kuboresha zaidi sekta ya mifugo kupitia njia mbalimbali huku ikiwa na nia ya kuona vijana wanafanya uzalishaji wa mali kwa kuingia katika sekta ya mifugo.

Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega amebainisha hayo katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madume ya ng’ombe 36 aina ya boran Heifer kwa Halmashauri ya Buchosa.

Amesema lengo la serikali ni kuona vijana wanafanya uzalishaji wa mali kwa kuingia katika sekta ya mifugo na kupeleka mifugo hiyo sokoni.

Wanawake waingia vitani uharibifu vyanzo vya majiWanamshauriwa vibaya Rais: Kitwanga‘’Nchi yetu ina ng’ombe milioni 33 na bado tija ipo chini sana kutokana na viwanda vingi havipati malighafi ya kutosha. Mifugo inatakiwa kuongeza tija na pato la taifa na kwa mtu mmoja mmoja,’’ Amesema Ulega.

Aidha, ameongeza kuwa kupitia programu maalum ya Samia Ufugaji kwa Tija (SAUTI), Serikali imefanikisha kuanzisha mafunzo ya unenepeshaji mifugo ambapo takriban vijana 70 wanapatiwa mafunzo hayo kwa vitendo katika Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Wilayani Misungwi.

Waziri Ulega amesema, serikali imeanzisha vituo atamizi vya SAUTI ambapo mpaka sasa kuna vituo nane kwa ajili ya vijana kufunzwa na kwamba kupitia vituo hivyo atamizi vijana watafundishwa namna bora na kisasa ya kutengeneza mashamba ya malisho na upatikanaji wa mifugo bora.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga aliishukuru serikali kwa kuipatia Halamshauri hiyo ya Buchosa Ng’ombe, huku mmoja wa wanafunzi hao akiishukuru serikali kwa kuja na programu hiyo ya ufugaji ambayo itawasaidia kupata ajira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live