Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaonya wavamizi maeneo ya hifadhi

Fd4118fbab08fb571a45ea008f0fa946.jpeg Serikali yaonya wavamizi maeneo ya hifadhi

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro, Hanji Godigodi amewaonya wananchi wanaovamia maeneo ya hifadhi kwa kuwataka kuheshimu mipaka iliyowekwa vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.

Godigodi alitoa onyo hilo alipotembelea Kijiji cha Iduindembo, Kata ya Utengule na kujionea baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walivyovamia eneo la hifadhi na kukata miti eneo lenye umbali wa zaidi ya kilometa 30. “Ndugu zangu wana Utengule niwaombe tuwe na subira, tusubiri ripoti msivamie eneo la hifadhi, zingatieni sheria, kanuni na maelekezo ya serikali… nimefika hapa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya nimekuja kuwasihi acheni kuvamia maeneo ya hifadhi tusubiri, serikali ya awamu ya sita ina nia njema na ninyi,” alisisitiza Godigodi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Idui ndembo, Deo Kungu pia alionya uvamizi eneo la hifadhi kwa kukata miti akisema vitendo hivyo havipaswi kufumbiwa macho. Aliomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya yeyote atakayebainika kuvunja sheria. Kungu alisema maeneo ya hifadhi yamekuwa yakivamiwa na wananchi kutokana na wingi wa mifugo na wakazi hususani kwenye vijiji vya Utengule, Iduindembo, Ndefi na Ngalimila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live