Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaongeza uwekezaji gesi asilia

Gesi Urusii.jpeg Serikali yaongeza uwekezaji gesi asilia

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma imesema kitendo cha serikali kuongeza hisa kwenye sekta ya gesi asilia kumefanya nchi kunufaika zaidi na rasilimali hiyo inayotarajiwa kukuza uchumi wa taifa.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma Deus Sangu,walipotembelea viwanda vya kuchakata gesi asilia cha Mnazibeyi na Madimba katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada nyingi hasa uwekezaji uliofanyika februari 24 nanimeingia katika rekodi ya nchi ambapo shirika la maendeleo ya petrol nchini (TPDC) imeongeza hisa 20% na kufanya shirika hilo linakuwa na umiliki wa 40% na 60% zinabaki za mwekezaji.

Aidha amesema kwa kuchukua 40% za hisa sasa inafanya TPDC kuwa na sauti kwasababu hapo awali walipokuwa na hisa ya 20% hawakuwa na maamuzi yoyote zaidi ya mshirika mwenza ambae ni kampuni.

Hata hivyo kitendo cha serikali kuongeza hisa kwenye sekta hiyo kumefanya nchi kunufaika zaidi na rasilimali hiyo inayotarajiwa kukuza uchumi ambapo kwasasa serikali imewekeza kwenye gesi asilia kiasi cha fedha shilingi bilioni 104.6 kwa nchi nzima.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Vuma Agustino, ameipongeza serikali kwa kuchukua hatua ya kuwasomesha vijana nje ya nchi ambao kwasasa ndio wanao simamia mitambo hiyo ya kuchakata na kuzalisha gesi.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TPDC Balozi Ombeni Sefue amesema watahakikisha rasilimali hiyo inatumika kubadili maisha ya watu pale ambapo gesi asilia inapatikana na kutoa mchango mkubwa kwa uchumi wa taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live