Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaondoa tozo 42 za kahawa

Kahawa Pc Serikali yaondoa tozo 42 za kahawa

Wed, 30 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza uamuzi wa Serikali wa kuondoa tozo 42 kati ya 47 ambazo walikuwa wanatozwa wakulima wa kahawa wa Mkoa wa Kagera hadi kufikia tozo 5 ambazo zitakuwa ni jumla ya Sh267 kwa kilo kutoka Sh830 za awali.

Waziri Mkuu ametoa maamuzi hayo kufuatia tume maalum aliyoiunda ili kupitia utaratibu na mfumo wa uendeshaji wa vyama vya ushirika wa zao hilo mkoani Kagera.

Majaliwa amewaagiza viongozi wa vyama vya ushirika kusimamia vyama vyao kwa uaminifu na weledi ili view na tija kwa wakulima.

Pia, Majaliwa amewata viongozi wa vyama hivyo kuacha tabia ya kukopa pesa benki kwa ajili ya kununua kahawa kwa wakulima.

Majaliwa ametoa maagizo hayo jana Jumanne Machi 29, 2022 wakati akiendesha mkutano maalum wa wadau wa zao hilo uliofanyika mkoani Kagera.

Amesema kuanzia sasa mauzo ya kahawa katika mkoa huo yatafanyika kwa njia ya mnada, utakaofanyika katika ngazi ya vyama vya msingi.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema baadhi ya vyama vya ushirika vimekuwa vikiwaumiza wakulima wa kahawa kwa kuwaongezea tozo zisizokuwa na tija.

Amesema jambo hilo linafanyiwa kazi kwani wakulima wa kahawa mkoani humo wamekuwa wakilia na tozo kubwa zaidi ya 47 na bado wamekuwa wakicheleweshewa malipo.

Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa kugawa miche ya kutosha ya kahawa kwa wakulima ili ilete tija na kuwaongezea kipato.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live