Kauli hiyo ameitoa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Generali Marco Gagut katika mkutano mkuu wa 27 wa Chama kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala Cooperative Union (TANECU) uliofanyika Wilayani Tandahimba.
“Tunafanya uhamasishaji mkubwa ili kuongeza uzalishaji wa korohso, lakini zinabaki majumbani. Lazima tujiulize kwanini wakulima hawaleti kwenye maghala na kuziuzia kwenye njia ambazo hazikubaliki ambao sio mfumo rasmi hivyo kushindwa kupata takwimu sahihi za uzalishaji wa korohso mkoani Mtwara,” amesema.
Naye Mwenyekiti wa chama cha msingi cha Bandarini, Ahmad Halfan ametaja sababu ya wakulima kuuza korosho kienyeji kuwa ni bei kuwa chini.
“Unajua ni ngumu kupata takwimu halisi ya uzalishji wa koroso kwa kauwa korosho zinazobakia majumbani hazitolewi taarifa hivyo kushindwa kufikisha taarifa Ili tupate takwimu sahihi minada isiwe ya kushuka ili kumvutia mkulima kupeleka ghalani,” amesema Halfan
“Kweli tunakosa uzalishaji mkubwa kwakuwa pembejeo hazifiki kwa kwa wakti mwaka jana ilichelewa ingawa uzalishaji ulipanda kidogo tumepata tani 35,000. Kwa hiyo Serikali iangalie nambna ya kubboresha zao la korohso,” amesema Halfan.
Advertisement Kwa upande wake Mustapha Mmanachoyo kutoka chama cha Msingi Rumana kilichopo wilayani Newala amekiri kuwepo kwa wakulima walioficha korosho nyumbani.
“Wakulima wengi wamebaki na korosho majumbani kwa sababu hawakuridhiswa na bei na pia bei ya pembejeo zilikuwa juu. Hali ambayo imewalazimu kuziacha nyumbani kuzioka na kuziuza kwa Sh12,000 hadi Sh13,000 kuliko kuuza kwenye minada kwa Sh1,500 hadi Sh1,600 huku makato yakiwepo zaidi ya Sh270,” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred amesema kuwa katika msimu huu wakulima wengi wamebakiza korosho majumbani za kubangua.
“Wakulima wanazo korosho ambazo hawajapeleka sokoni wameziweka kwa ajili ya kubangua ni jambo zuri kikubwa sisi tutahakiksha tunafahamu kiasi cha korosho kilichopo majumbani ili kupata takwimu,” amesema Alfred