Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakusudia kutoa mafunzo kwa wavuvi

Uvuvi 23 Serikali yakusudia kutoa mafunzo kwa wavuvi

Tue, 25 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Hayo yalisemwa na Waziri wa Uvuvi na Uchumi wa Bluu, Abdalla Hussein Kombo, wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka, Issa Haji Ussi, aliyetaka kujua lini serikali itaanza kutoa elimu ya uchumi wa bluu kutokana na dhana hiyo kuwa mpya kwa wananchi.

Kombo alisema wanakusudia kuanza kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kuanzia kwa wavuvi wa mwambao wa pwani kwa ajili ya kufahamu dhana ya uchumi wa bluu na vipi wananchi watanufaika kuvuna rasilimali ziliomo baharini kiuchumi.

Alisema wiki ijayo wanakusudia kuwakutanisha wadau katika kongamano litakalowakutanisha wavuvi wa Unguja na Pemba na kuelezea faida zitakazopatikana katika serikali kuingia uchumi wa bluu ambao umelenga kuwanufaisha wananchi kiuchumi.

“Mheshimiwa Spika nakubaliana na Mwakilishi ni kweli dhana ya uchumi wa bluu ni mpya, lakini wananchi ikiwamo wavuvi wengi hawaifahamu kikamilifu kwa hivyo wizara imejipanga kuwafikia walengwa kwa ajili ya kunufaika ikiwamo kuzingatia uvuvi haramu,” alisema.

 

 Alisema uchumi wa bluu utazingatia zaidi utunzaji wa mazingira ya baharini kwa ajili ya kunufaika na rasilimali ziliomo ikiwamo kupambana na uvuvi haramu.

“Mheshimiwa uchumi wa bluu malengo yake makubwa utakuwa ukizingatia utunzaji wa rasilimali za baharini kwa kutunza matumbawe ya baharini ambayo ndiyo mazalia ya samaki,” alisema Kombo ambaye ni mtaalamu wa masuala ya usalama wa baharini na mikataba ya kimataifa.

Chanzo: ippmedia.com