Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakusanya Tsh. bilioni 66 daraja la Kigamboni

DARAJA Kigamboni.jpeg Daraja la Kigamboni

Fri, 17 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema kuanzia Julai Mosi, 2022 utaratibu wa kulipa tozo katika mfumo mpya utaanza kwenye daraja la Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolea bungeni leo Ijumaa Juni 17, 2022 na naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile.

Mbunge huyo ameomba kujua mfumo mpya wa kulipia gharama hizo kwa siku, wiki hadi mwezi utaanza lini kwenye daraja hilo muhimu kwa wakazi wa jimbo lake.

Katika swali la msingi, Dk Ndugulile ameuliza ni kiasi gani cha fedha kimekusanywa tangu daraja hilo kuanza kutumika na Serikali ina mpango gani wa kufanya huduma ya daraja hilo kuwa bure.

Akijibu swali hilo, Kasekenya amesema mfuko wa NSSF ulianza kupokea fedha zitokanazo na tozo kwa watumiaji wa daraja Mei 14, 2016 baada ya kuzinduliwa.

Naibu Waziri amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei,2022 mfuko ulikuwa umekusanya Sh66.86 bilioni.

“Serikali imeendelea kupunguza tozo kwa watumiaji wa daraja hilo tangu kuzinduliwa kwake kwa kuzingatia tathmini ya uwezo wa wananchi kumudu tozo hizi,” amesema Kasekenya.

Amesema mara ya mwisho Serikali kupunguza tozo husika ilikuwa Mei 21, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live